Maktaba ya mapishi

Kuku wa sweet and sour

KichinaMlo mkuu 5 watu 45 dakika
Kuku wa sweet and sourKuku wa sweet and sour

Add the chicken at the end so it stays crispy. Sweet and Sour Chicken — a East Asian recipe for 5 people with full ingredients, quantities and step-by-step instructions in Kiswahili and English. Ready in about 45 minutes.

Mahitaji

  • Kuku1 kilo
  • Soya sauce2 vijiko vikubwa
  • Unga wa mahindi4 vijiko vikubwa
  • Siki3 vijiko vikubwa
  • Mayai1 idadi
  • Pilipili hoho2 idadi
  • Vitunguu maji1 idadi
  • Nanasi1 idadi
  • Sukari4 vijiko vikubwa
  • Tomato sauce4 vijiko vikubwa
  • Kitunguu swaumu2 vijiko vidogo
  • Mafuta ya kupikia12 vijiko vikubwa
  • Viazi mviringo (kwa chipsi)1 kg

Hatua za kupika

  1. 1Kata kuku vipande, changanya na yai na unga wa mahindi.
  2. 2Kaanga kwenye mafuta mengi hadi awe wa dhahabu; mtoe, mweke kwenye karatasi.
  3. 3Changanya siki, sukari, tomato sauce, soya sauce na kikombe nusu cha maji.
  4. 4Kaanga kitunguu swaumu, kitunguu na pilipili hoho dakika 3 - visilainike sana.
  5. 5Mimina mchanganyiko wa sauce; chemsha hadi uwe mzito.
  6. 6Weka nanasi na kuku; changanya haraka na uzime moto.
  7. 7Pakua na chipsi.

Maelezo

Kuku aingie mwisho ili abaki mkavu.

Hujui cha kupika wiki hii?

Acha Tupike Nini ikupangie. Weka pishi hili kwenye mpango wako wa wiki, tengeneza orodha ya manunuzi na tuma kwa WhatsApp.